Rapa 6ix9ine Amelazwa Hospitali Baada Kuripotiwa Kupigwa

Rapa 6ix9ine Amelazwa Hospitali Baada Kuripotiwa Kuvamiwa Na Kupigwa Na Kundi La Watu Akiwa Gym Huko Kusini Mwa Florida. Amejeruhiwa Kwenye Taya, Mgongo Pamoja Na Ubavu

Wakili Wa 6ix9ine, Lance Lazzaro Ameiambia TMZ...."6ix9ine Alikuwa Ndani Ya Gym Ya Sauna Wakati Tukio Lote Hilo Linatokea La Kuvamiwa Na Watu Hao, Hata Hivyo Alijaribu Kupambana Nao Lakini Walikuwa Wengi Na Hakuwa Na Ulinzi (Bodyguard) Kwa Wakati Huo". Wafanyakazi Wa Gym Walisikia Zogo Na Kutoa Taarifa Kwa Meneja Lakini Pia Jeshi La Polisi Na Ems Waliitwa Na Eneo La Tukio Kisha Kumkimbiza 6ix9ine Hospitali Na Ambulance

Hatua Inayofuata, Wakili Lazzaro Anasema Kwamba Amepanga Kuita Polisi Kuhakikisha Kwamba #Tekashi69 Anapata Ulinzi Anaouhitaji. Kumbuka Aliachiwa Huru Kutoka Jela 2020 Baada Ya kuwa-Snitch Members Wenzake Wa "Nine Trey Gangsta Bloods" Ili Waende Jela, Lakini Bado Haijajulikana Kama Uvamizi Huo Unahusiana Na Masuala Yake Ya U-Snitch. Kama Unakumbuka Rapa #Tekashi69 Baada Ya Kutoka Jela Ilimlazimu Kuingia Utaratibu Maalumu Wa Kulindwa Na Serikali Baada Ya Kutoa Ushahidi Mahakamani (Witness Protection) Kwa Kuhofia Maisha Yake.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii