Stamina "Wanaume tunaongoza kwa usaliti"

Msanii wa muziki wa Hip hop Stamina Shorwebwenzi ambaye ndoa yake ilidumu kwa miezi 7 amefunguka ya moyoni kueleza jinsi vijana wengi wanavyopitia magumu kwenye maisha ya ndoa.


Rapa huyo amedai yeye baada ya kuachana na aliyekuwa mke wake ndipo alivyoziocha changamoto za ndoa yake huku akidai kwamba wakati yupo ndani ya ndoa alikuwa haoni kasoro yoyote.

“Mimi nikiwaona watu wanafanya anniversary ya miaka 15 nawapongeza sana. Nimegundua ndoa inahitaji vitu vingi sana, mimi baada ya kutoka ndani ya ndoa ndio nimejua umuhimu wa ndoa, yaani baada yakutoka nimekuja kugundua ndoa ina

Aliongeza, “Kwa mfano hili suala la usaliti, wanaume sisi tunaongoza kwa usaliti, nikipiga mahesabu ya haraka haraka hata kwa marafiki zangu nawaona changamoto zao, ila sijawahi zisema kwa mashemeji. Nikipiga mahesabu yangu wanaume tunaongoza ila mwanamke akija kusaliti mara moja, mwanaume hawezi vumilia. Kwahiyo kumbe sisi tunafanyaga vitu ambavyo sisi hatupendi fanyiwa,”

Stamina ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Machozi’ amesema kwasasa amegundua ndoa yake kuvunjika kulisababishwa kwa kukosa uvumilivu na kama angevumilia basi mpaka sasa angekuwa na mke wake.

Amedai kitu ambacho kimechangia ndoa yake kuvunjika ni familia za pande zote mbili kushindwa kuelewana.

hitaji hichi na hichi,” Stamina alisemaPata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii