Klabu ya Crystal Palace imempiga kalamu kocha mkuu Patrick Vieira baada ya kuiongoza klabu hiyo kwa mechi 12 zilizopita bila kusajili ushindi wowote.
Palace haijashinda mechi yoyote katika mwaka 2023 na walipigwa 1-0 na Brighton katika mechi ya Ligi Kuu ya Uingereza mnamo Jumatano, hiki kikiwa kipigo chao cha tatu kwa mpigo. Crystal Palace inashikilia nafasi ya 12 kwenye jedwali la EPL, zikiwa ni alama tatu pekee mbele ya Bournemouth wanaoshikilia nafasi ya 18 na wana mechi moja zaidi ya kucheza.