Mwanamuziki Costa Titch Afariki Akitumbuiza Jukwaani

Afrika Kusini inaomboleza kifo kingine cha mwanamuziki maarufu. Kwa mujibu wa taarifa za mitandao ya kijamii, rapa Costa Tsobanoglou maarufu kwa jina la kisanii Costa Titch, ameripotiwa kufariki dunia.

Rafiki yake wa karibu Junior De Rocka, alisambaza habari hizo kwenye akaunti yake ya Instagram. Alishiriki upya chapisho lake na kuandika “RIP Bro.”

Kwa mujibu wa taarifa ambazo hazijathibitishwa, rapper huyo alianguka jukwaani kwenye tamasha la Ultra Afrika Kusini, kwenye ukumbi wa Expo Centre mjini Nasrec, Johannesburg.

Mbali na hilo msanii wa muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz amepost inst story yake na kuandika Daaaah.

Coata Titch amewahi kufanya ngoma na Diamond Super Star lakini pia na Mbosso Shetani.

Bado hakuna taarifa zozote rasmi zilizotolewa na Bongo Five tutakuletea taarifa zitakapojitokeza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii