Shilole atumia zaidi ya Tsh Mil. 90 kuurudisha mgahawa

Msanii wa muziki na Mjasiliamali, Shilole amefanikisha kuurudisha mgahawa mpya wa Shishi Food Mabatini, Kijitonyama jijini Dar Es Salaam baada ya ule wa awali ambao ulikuwa maeneo ya Leaders Club jijini Dar Es Salaam kuvunjwa ili kupisha ujenzi wa Zahanati.

Mume wa Shilole, Rommy amedai haikuwa rahisi kufanikisha hilo kwani wamewekeza zaidi ya Tsh Milioni 90 katika ujenzi huo mpya huku wakiwa wanatoka kwenye kubomoa mgahawa wao wa Leaders Club ambao waliwekeza pesa nyingi.

Rommy amedai kutokana na sakata hilo amegundua mke wake ni mpambanaji haswa kwani yeye alimkimbia baada ya sakata la bomoabomoa kuchanganya kwani walikuwa wanatofautiana kwenye baadhi ya mambo akaona akimbilie Dodoma.

Amedai zoezi lote la bomoabomoa yeye alikuwa yupo Dodoma kuepuka kukaa na msanii huyo ambaye alikataa ushauri wake.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii