Xi Jinping achaguliwa tena kuongoza muhula wa tatu

Rais wa China, Xi Jinping amechaguliwa tena kwa kauli moja kuwa rais wa Taifa hilo hi leo Ijumaa Machi 10, katika kura ya wabunge na ataongoza China kwa muhula wa tatu wa miaka mitano, jambo ambalo halijawahi kutokea nchini humo.


Xi Jinping yuko madarakani kwa miaka kumi tangu 2013, na hakukuwa na shaka yoyote juu yakeambapo Mwanasiasa huyo mwenye umri wa miaka 69 tayari alipata nyongeza ya miaka mitano.

Oktoba 2022 alichaguliwa kuwa Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha CCP na mwenyekiti wa tume ya kijeshi, nyadhifa ambazo ni mbili muhimu zaidi za madaraka nchini humo.

Kuchaguliwa kwake tena ni kilele cha ongezeko ambalo limemfanya kuwa kiongozi mwenye nguvu zaidi nchini China tangu vizazi kadhaa kupita na hivyo kuweka historia mpya.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii