BEKI WA KAZI SIMBA AREJEA

HENOCK Inonga, beki wa Simba amerejea kwenye uimara wake taratibu baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons.

Katika mchezo huo wa ligi Inonga mwenye mabao mawili alikwama kuyeyusha dakika 90 wakati timu hiyo ikisepa na pointi tatu mazima.

Hakuwa kwenye mchezo dhidi ya Dodoma Jiji na Coastal Union na anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji watakaocheza dhidi ya Singida Big Stars, Februari 3,2023 Uwanja wa Mkapa.

Beki huyo wa kazi ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye mazoezi Februari Mosi, Uwanja wa Bunju Arena chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira.

Kwenye mazoezi hayo Inonga alikuwa akishirikiana na wachezaji wengine ikiwa ni pamoja na Pape Sakho, Kennedy Juma na Mzamiru Yassin kutimiza majukumu yao.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza ubao wa Uwanja wa Liti ulisoma Singida Big Stars 1-1 Simba.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii