Mtoto wa Shilole Amuheshimisha Mama yake, Agonga 'Division one' Kidato cha nne

Shilole ambaye yeye binafsi hakuwahi kufika hata kidato cha nne sababu ya kukumbana na changamoto za kimaisha katika umri mdogo, amejitosa kusherehekea mwanae kufaulu vizuri kwa kupost picha hiyo kisha kuandika kwa hisia.


“Labda kwa walio zoea wanaweza ona kawaida. Lakini kwangu mimi Shilole ambae sikufikia elimu ya namna hii na kama mama ambae napambana kuwapa wanangu elimu bora ili wao wafike mbali na wapate maisha mazuri ambayo mm sikupata, BASI HII KWANGU NI KUBWA MNOOOO.


Binti yangu wa pili Rahma amenifurahisha mwenzenu matokeo yake ya kidato cha nne kanipigia Div ONE yake saafi. Asante mwanangu mama yenu nawapambania na mnanipa moyo mnoo na mnanitoa machozi ya furaha sana. Mungu nakushukuru sana kwa hili.


Asante uongozi wa shule ya St. Christina kwa ushirikuano na juhudi zenu. Rahma tulikubaliana hakuna simu mpk umalize form 4 tena ufaulu. Sasa naona umeipambania zawadi yako mwanangu sina budi kujitahid kutimiza ahadi yangu , Bilnass jiandae Leo nina furaha sana Alhambdulillah” ameandika Shilole.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii