Wanafaidi Matunda ya Kumvumilia Arteta

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola anaamini kuwa viongozi wa Ligi Kuu ya Uingereza Arsenal sasa wanafaidi matunda ya kumvumilia Mikel Arteta kama kocha wao kwa miaka mitatu. 

Arteta alihudumu kama naibu wa Guardiola katika klabu ya Manchester City kwa miaka mitatu na nusu kabla ya kuchukua mikoba ya ukufunzi ugani Emirates mwaka 2019 - hii ikiwa ni mara yake ya kwanza kuwa kocha mkuu. 

"Pongezi kubwa kwa Arsenal ni kumuunga mkono katika hali mbaya na kumwamini, kubaki naye na kumtegemea. Mwisho wa siku, unahitaji muda, unahitahi uekezaji na matokeo yako hapa. Ni changamoto kwetu kuwapa changamoto," Guardiola amesema. 


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii