Dr Mwaka Agoma Kuachwa, Licha ya Masheikh Kuvunja Ndoa Hiyo

Dr.Mwaka hajakubali kuachwa ageuka mbogo, adai yeye hajatoa talaka kwa Queen na atamshitaki
mtu yeyote anakayejitosa kumuoa, awalipua masheikh wa mkoa

Dr Mwaka amegeuka Mbogo baada ya ndoa yake na mkewe Queen Masanja kuvunjwa na Balaza la Masheikh wa mkoa wa Dar es salaam.

Dokta Mwaka anadai taratibu zilizotumika ni za kihuni na yeye hayupo tayari ndoa yake kuvunjwa na wahuni huku akieleza kwamba kisheria mwenye mamlaka ya kuvunja ndoa kidini ni Kadhi peke yake.

Aidha Mwaka amesema ni kweli hawana maelewano mazuri na mke wake, lakini hakubaliani na maamuzi yaliyolewa na viongozi wa kidini (Masheikh wa mkoa wa Dar es salaam) ambapo amesema yeye bado anamtambua Queen Masanja kama mke wake wa halali na yeyoye atakayejitokeza kumuoa atamchukulia hatua kali za kisheria kwani atakuwa ameoa mke wa mtu.

Ikumbukwe, ndoa ya Dokta Mwaka na mkewe Queen Masanja ilivunjwa rasmi Jumatano ya Januari 25, 2023 ambapo ndoa hiyo ilivunjwa baada ya kikao cha kamati ya Masheikh wa mkoa wa Dar es salaam chini ya Mwenyekiti Sheikh wa Mkoa, Alhaji Mussa Salum kuketi kwa dharura na kuridhia maombi ya Queen kutaka apewe talaka

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii