MIONGONI mwa taarifa ambazo zilikuwa na sarakasi nyingi ni pamoja
usajili wa nyota Mohamed Issa Banka kuibuka ndani ya Ruvu Shooting na
kabla ya kuanza kucheza mkataba wake ukavunjwa.
Banka ambaye amewahi kukipiga ndani ya kikosi cha Yanga, Namungo na
Mtibwa Sugar alipaswa kuwa ndani ya kikosi cha Ruvu Shooting kwenye
mzunguko wa pili katika dirisha dogo
Nyota huyo alipewa dili la miezi sita na alikubali kusaini tatizo
ikaja kwenye kuripoti kambini kuanza majukumu yake mapya kabla ya kuanza
kucheza hata mchezo mmoja mkataba ukavunjwa.
Taarifa iliyotolewa na Ruvu Shooting, Januari 24,2023 ilieleza namna
hii:”Uongozi wa Klabu ya Ruvu Shooting tumefikia makubaliano kwa pande
zote mbili ya kuvunja mkataba kati yetu na mchezaji Mohamed Issa Banka
ambaye ameonesha utovu wa nidhamu wa kutowasili kambini tangu asajiliwe.
“Kwa sasa hayupo kwetu alipaswa kujiunga nasi dirisha dogo la usajili,”.
Nyota huyo alitambulishwa ndani ya Ruvu Shooting kuwa mwanafamilia
mpya Desemba 31,2022 na kutangazwa kufikia makubaliano kuvunja mkataba
Januari 14,2023.