• Alhamisi , Disemba 4 , 2025

Wazee washauri wasiotunza wazazi washtakiwe

Wazee Mkoani Lindi wameitaka Serikali kupitisha sheria ya mzazi kumshtaki mtoto wake endapo atamtelekeza bila kumpatia msaada wowote huku wakisema katika nyakati hizi za uzee wanahitaji usimamizi na msaada kwakuwa hawana nguvu tena ya kuhangaika kama zamani. 


Hayo yamezungumzwa katika kikao cha Baraza la Wazee mkoani Lindi ambapo Wamesisitiza kuwa kwa tamaduni za kiafrika jitihada za mzazi kumtunza mtoto hazitakiwi kupotea bure ni wajibu pia wa watoto kuwalea wazazi wao

Nayo tabia ya vijana kuzaa na kutelekeza watoto wao kwa wazazi imeonywa, kwani wazee wengi mkoani Lindi wanaonekana kuwa na maisha magumu na mara kadhaa huwatumia watoto hao kwenye kuomba misaada majumbani.

Aidha hoja ya kujenga vituo kwaajili ya kulea wazee imeonekana sio nzuri kwani wazazi wana watoto wanaoweza kuwamudu hivyo kumuweka mzazi kituoni ni jambo la aibu na huashiria thabiti kuwa wazee wameshindwa kusaidika.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii