Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Ardhini (Latra) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini imesema inaendelea na ukaguzi wa mabasi ya kwenda mikoani ili kubaini yanayozidisha nauli na kuchukua hatua.
Ofisa Mfawidhi wa Latra, Denis Daudi ameyasema hayo leo, Desemba 30,2021 na kueleza kuwa ukaguzi huo umeanza kabla ya kuanza kwa msimu wa sikukuu za Krismasi na mwaka mpya na kuongeza kuwa Latra itahakikisha inadhibiti kupandishwa kwa nauli kiholela.
Ameongeza kuwa ukaguzi unafanywa alfajiri kuanzia katika kituo kikuu cha mabasi ya mikoani na vituo vya ukaguzi katika mpaka wa Igawa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya na Mji wa Makambako Mkoa wa Njombe.