Diddy Amchana Burna Boy "Nilikusaidia Ushindi Grammy Mwaka Jana, Mwaka Huu Ulizani Utashinda Grammy Bila Mimi? "

Rapa Diddy amekanusha uvumi wa kuwa amemchana Burna Boy baada ya kushindwa kuondoka na Tuzo ya Grammy mwaka huu. Taarifa hiyo ilionekana mitandaoni ikionesha imetoka kwenye insta story ya akaunti ya Diddy ikimchana Burna kuwa amekosa Tuzo baada ya kuamua kufanya Album nyingine bila uwepo wa Diddy.

Kwenye moja ya comment zake hapa instagram, Diddy ambaye alikuwa Executive Producer wa Album ya Burna Boy (Twice As Tall) iliyoshinda Grammy 2021, alikanusha uvumi huo kwa kusema hakuna ukweli wowote.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii