Kocha Mkuu wa Simba C Roberto Oliviera ‘Robertinho’, amempigia Saluti Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chotta Chama kwa kiwango kizuri alichokionesha dhidi ya Singida Big Stars na Al Hilal ya Sudan.

Chama alikuwa sehemu ya wachezaji waliochagiza ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Singida Big Stars Ijumaa (Februari 03), huku akisaidia matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Al Hilal jana Jumapili (Februari 05), Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kocha Robertinho amesema Chama ni mchezaji mzuri mwenye maarifa na kwenye michezo hiyo amecheza katika kiwango cha juu sana, akiwa nguzo imara ya mafanikio ya kikosi chake.