KIPA SIMBA SC AINGIA ANGA ZA AZAM FC

Inaelezwa  kuwa Klabu ya Azam FC ipo kwenye hesabu za kuinasa saini ya kipa namba mbili wa Simba, Beno Kakolanya.
Mkataba wa kipa huyo ambaye aliongeza hivi karibuni miaka miwili unatarajiwa kugota ukingoni hivi karibuni.


Taarifa inaeleza kuwa Beno ameahidiwa mshahara mkubwa zaidi ya anaolipwa ndani ya Klabu ya Simba pamoja na uhakika wa kuanza ndani ya kikosi cha kwanza cha Azam endapo atajiunga nao.


Kwa sasa timu hiyo kipa wake namba moja ni Ali Ahamada ambaye ameanza kikosi cha kwanza kwenye mechi 14 msimu wa 2022/23.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii