Zaidi ya wahamiaji 400 waokolewa baharini

Meli ya shirika lisilo la kiserikali la Ujerumani Sea-Watch 3, ikiwa na wahamiaji 444, ilikuwa ikingoja kupewa bandari ya usalama kutia nanga baada ya operesheni  tano za uokoaji kutekelezwa katika Bahari ya Mediteranian.

Meli ya shirika lisilo la kiserikali la Ujerumani Sea-Watch 3, ikiwa na wahamiaji 444, ilikuwa ikingoja kupewa bandari ya usalama ya kutia nanga siku ya Jumanne baada ya operesheni tano za uokoaji kutekelezwa katika Bahari ya Mediteranian.

Siku ya Krismasi , wafanyakazi wa meli hiyo waliwaokoa wahamiaji 257 kutoka kwenye boti za mbao zilizojaa katika eneo la operesheni katika maji ya kimataifa kwenye pwani ya Libya.

Mapema asubuhi ya mkesha wa Krismasi waokoaji waliwaokoa watu 93 wakiwemo watoto wengi waliokuwa peke yao kutoka kwenye mashua ya mbao iliyokuwa hatarini katika maji ya kimataifa kusini mwa kisiwa cha Italia cha Lampedusa.

Wiki iliyopita pekee, takriban watu 160 walikufa maji katikati mwa bahari ya Mediteranian walipokuwa wakijaribu kukimbia, kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii