Philemon Mulala Auawa na Mbwa Wake 3 Afrika Kusini

Nyota wa zamani wa Chipolopolo, Philemon Mulala ameuawa na mbwa wake watatu nyumbani kwake Lichtenburg, Afrika Kusini. 


Mulala aliumwa na mbwa hao alipotoka nje kuchunguza sababu yao kubweka sana baada ya umeme kukatika.

Mke wake aliwaambia maafisa wa kwamba alisikia mbwa wakibweka lakini hakujishughulisha kwenda kuangalia kilichokuwa kikiendelea.

Alipuuza kwa sababu mbwa hao mara kwa mara walikuwa wakiwabwekea wapita njia na magari yaliyokuwa yakipita.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii