Klabu ya Arsenal imefunguliwa mashtaka na Shirikisho la Soka nchini Uingereza (FA) kuhusu mwenendo wa wachezaji wake katika mechi yao ya Ligi Kuu ya Uingereza na Newcastle United
Kwa mujibu wa FA, Arsenal ilikosa kuwadhibiti wachezaji wake katika sare hiyo ya 0-0 na Magpies mnamo Jumanne - Januari 3 - ugani Emirates.
Arsenal walitazama kwa machungu kilio chao cha kupewa penalti kikikataliwa na refa mara mbili katika dakika za mwisho za mechi hiyo.
Vijana wa kocha Mikel Arteta wamlikimbilia na kumzunguka refa Andrew Madley wakitaka kupewa penalti wakidai mchezaji wa Newcastle alikuwa ameunawa mpira kwenye kisanduku.