Thierry Hitimana amevunja mkataba wake na klabu ya Simba kama kocha msaidizi baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Hitimana jana Disemba 28 amewaaga wachezaji wa timu hiyo jioni hii wakiwa katika mazoezi kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam.
Hitimana aliwasili mapema uwanjani hapo akiwa na gari aina ya Toyota Wish kabla ya wachezaji ambapo nao waliwasili dakika chache baadae ambapo katika muda wa kusali alitumia pia kuwaaga kabla ya kuondoka Uwanjani hapo.