Messi na Cristiano itakuwa mechi yao ya mwisho kukutana 2023 ?

Paris Saint-Germain ikiwa na Lionel Messi itasafiri hadi Saudi Arabia kwajili ya mchezo wa kirafiki  Januari 19 dhidi ya kikosi kitakachojumuisha wachezaji wa Klabu ya Al Hilal na Al Nassr ambayo imemsajili Cristiano Ronaldo.

Endapo mechi hiyo itathibitishwa na wachezaji wote wawili wakaitwa kwenye kikosi basi huwenda ikawa ndiyo nafasi ya mwisho kwa mastaa hao Lionel Messi na Cristiano Ronaldo kucheza pamoja kabla ya kustaafu kwao.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari,  Achraf Ben Ayad mechi hiyo ilipangwa kupigwa mwanzoni mwa mwaka 2022 kabla hata ya ujio wa Ronaldo lakini ilivunjika kutokana na janga la Corona.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii