Msanii wa bongo fleva Harmonize ametangaza kuwa kila mtu ambaye atataka kufanya nae kolabo lazima atoe hela ndipo ataweza kufanya kolabo.
Ikiwa baadhi ya wasanii wao hawako tayari kufanya kolabo kwa hela na wengi wao wakieleza kuwa inakua ngumu sana kwa msanii anae taka hela baadae nae akitaka kolabo inakua changamoto kupata kolabo bila kumlipa msanii anaetaka kufanya nae kolabo.
Kwa upande Harmonize yeye amesema kuwa anaanza kutoza kiasi cha TSh. MILIONI 100 kwa ajili ya kufanya naye Kolabo, lakini sharti la kwanza wimbo uwe mkali.