Brazil na Ureno Zatinga Hatua ya 16-Bora Kwenye Kombe la Dunia

Brazil iliungana na Ufaransa katika hatua ya mwondoano kwenye Kombe la Dunia siku ya Jumatatu, Novemba 28, baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Switzerland.


Kiungo wa kati wa Brazil, Casemiro ndiye alifunga bao la kipekee ambalo liliwasadia washindi hao mara tano wa Kombe la Dunia kufuzu katika Kundi G.Huku Brazil hao wakikosa huduma za nahodha wao nyota Neymar aliyejeruhiwa, walionekana kana kwamba wangekuwa na ulazima wa kusawazisha kwa pointi moja baada ya bao la Vinicius Junior katika kipindi cha pili kukataliwa kwa msingi wa kuotea

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii