YANGA wagawa Dozi kwa Biashara 2-1

Kutoka pale Uwanja wa Mkapa, Wenyewe wanajiita ni Wananchi, Yanga SC, hii leo imeshuka Dimbani kuivaa Biashara United, huku Biashara United wakitangulia kutikisa nyavu za Wananchi kupitia Atupele Green Dakia ya 2, na kabla ya mapumziko Mwananchi wakasawazisha Goli kupitia Fiston Mayele Dakika ya 40 Huku Said Ntibazonkiza akiwapaisha kileleni zaidi Wananchi kwa mkwaju wa Penati, dakika ya 79

Mechi nyingine ilikuwa kati ya Kagera Sugar FC na Tanzania Prisons katika uwanja Kaitaba, ambapo wanatamu tamu hao wametembezewa kichapo cha Goli moja na wana jela jela kupitia Marco Muhilu dakika ya 78, na kuwafanya Tanzania Prisons kutoka na Pointi 3 Muhimu.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii