Shirikisho la vyama vya kandanda duniani FIFA kuichunguza timu ya Ujerumani

Shirikisho la vyama vya kandanda duniani FIFA litachunguza hatua ya timu ya Ujerumani ya kukiuka taratibu za kuitisha mkutano na waandishi habari kabla ya pambano na timu ya Uhispania. Bodi ya shirikisho hilo imefahamisha leo kwamba kamati yake ya nidhamu inachunguza kwa nini hakuna mchezaji yeyote aliyekutana na waandishi habari kabla ya pambano kulingana na kanuni za mashindano.

Ni kocha wa Ujerumani Hansi Flick tu aliyesema kwamba wachezaji waliepushiwa adha ya safari ndefu ya kwenda kwenye mkutano na wandishi habari siku moja kabla ya pambano la jana na Uhispania ambapo timu hizo mbili zilitoka sare bao moja kwa moja. Ujerumani inaweza kupewa adhabu ya kulipa faini au inaweza kupewa onyo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii