Klabu ya Saudi Arabia ya Al Nassr inatarajia kupata saini ya mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo mwishoni mwa mwaka huu.
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United atasaini mkataba wa miaka miwili na nusu wenye thamani ya £174m (KSh26.1 bilioni).
Kwa mujibu wa gazeti la Marca, kwa sasa mshambuliaji huyo hodari mwenye umri wa miaka 37, yuko nchini Dubai akitazamiwa kusafiri kuelekea Saudia. Ronaldo pia ameweka nyuma masaibu ya Kombe la Dunia na amemaliza mazoezi yake mjini Valdebebas nchini Uhispania.