CHADEMA waunda bunge lao

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CHADEMA John Mrema amesema Bunge la Wananchi limeundwa na wanachama wa chama hicho waliogombea ubunge mwaka 2020 na litakuwa linaendeshwa kwa njia ya mtandao na litashughulika na bajeti za serikali na mambo mengine ambayo Bunge la Jamhuri ya Muungano linafanya.

Mrema amesema kuwa, Bunge hilo lina nia ya kuwasilisha kero za wananchi kwenye serikali kuu na zipatiwe ufumbuzi, kwa madai ya kwamba wabunge waliopo bungeni hawafanyi jambo hilo.

"Wajumbe wa Bunge hili ni wale wagombea wa CHADEMA waliogombea katika majimbo katika uchaguzi mkuu uliopita, litakuwa linatoa maoni mbadala na kuishauri serikali kwenye mambo yote na litawafikia wananchi, na kero zote zitakusanywa na kuwasilishwa serikalini kwa njia mbalimbali," amesema Mrema


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii