ANC ya Afrika Kusini inafanya mkutano mkuu kuchagua kiongozi wa chama

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kinafanya mkutano wake mkuu leo ambao unatarijiwa kumchagua kwa mara nyingine rais Cyril Ramaphosa kuwa mwenyekiti licha ya kashfa iliyomchafulia jina kiongozi huyo wiki kadhaa zilizopita.

Ramaphosa anawania muhula mwengine wa uongozi wa chama hicho katika wakati ANC inakabiliwa na mivutano ya ndani na kupoteza uungaji mkono wa wapigakura kwenye historia yake ya miaka 28 ya kuwa madarakani.

Mwanasiasa huyo anayejinasibu kuwa mpinga rushwa alichukua hatumu za uongozi wa chama mwaka 2017 baada ya mtangulizi wake Jacob Zuma kuandamwa na kashfa nyingi za rushwa na ukiukaji wa maadili.

Hata hivyo taswira ya Ramaphosa nayo imeingia doa wiki chache zilizopita baada ya kutuhumiwa kuwa alificha taarifa za wizi wa kiwango kikubwa cha fedha uliotokea kwenye shamba lake huko Phala Phala.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii