Mrisho Mpoto Aondoka Nchini Kuelekea India Kutumbuiza Kwenye Tamasha

Mwanamuziki wa nyimbo za asili na uhamasishaji nchini Tanzania, Mrisho Mpoto ameondoka nchini  pamoja na bendi yake kuelekea nchini India katika tamasha kubwa la kidini na kiutamaduni ambalo tayari watu wapatao takribani milioni 15, wamethibitisha kuhudhuria tamasha hilo.

Tamasha hilo litafanyika kwa muda wa siku 38, huku Tanzania ikiwa ndiyo nchi pekee kutoka Afrika iliyochaguliwa kutumbuiza kupitia Mrisho Mpoto Band.

Akizungumza mbele ya vyombo la habari, akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Mpoto amesema kuwa wanatarajia kutoa burudani kila siku huku watu zaidi ya elfu 56, wakihudhuria onyesho lao ambapo pia watafanya ufunguzi mbele ya Rais wa India.

Mpoto amemshukuru sana Rais Dk Samia Suluhu Hassan, kwa kufanikiwa kufungua mipaka ya utalii nje ya nchi mpaka hivi sasa Tanzania inathaminika kwa kila nyanja.




Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii