Mchezaji anayelengwa na Arsenal, Chelsea na Manchester City Dusan Vlahovic huenda akaondoka katika klabu yake katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari kwasababu mshambuliaji huyo wa Fiorentina anataka kulipwa mshahara wa £200,000 kwa wiki. (Star)
Manchester United wamemtambua kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen mwenye umri wa miaka 18 Florian Wirtz - anayefahamika kuwa 'Kai Havertz' mtarajiwa kama mchezaji huru. (Express)
Kipa wa Aston Villa na Argentina Emiliano Martinez, 29, ni miongoni mwa makipa wanaolengwa na Manchester United ili kumrithi David de Gea, 31. (Star)