Amber Lulu Ndoa Yanukia

Msanii  wa muziki wa Kizazi Kipya Amber Lulu ambaye hatimaye ametangaza jambo zito, amesema ndoa yyake inanukia.


Amber Lulu ambaye ni mama wa mtoto mmoja aliyezaa na rapa Emba Botion ametangaza hatua hiyo baada ya kudaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu mpya.


Amber Lulu anasema kuwa, ataolewa hivi karibuni na kwamba halikuwa jambo ambalo alidhani litatokea.


“Naolewa. Asante Mungu, sijatarajia hili,” anasema Amber Lulu anayetamba na ngoma yake ya Halichachi.


Hivi karibuni Amber Lulu alidaiwa kuwa kwenye uhusiano mpya wa kimapenzi na jamaa f’lani.


Hii ni baada ya Amber Lulu kuposti picha ya kimahaba akiwa na msanii wa Bongo Fleva aitwaye The Dream na kunogesha tetesi za kuwa kwa sasa moyo wake umetulia kwa msanii huyo ambaye kwa muonekano ni mdogo kiumri zaidi yake.
Kabla ya hayo, Amber Lulu alikuwa ameposti picha yake na kudokeza kwamba alikuwa amepata mpenzi anayempenda mwanawe, Ariana.


Amber Lulu alisema kuwa, kabla ya hapo alikuwa akipitia ukatili kutoka kwa baba wa mtoto wake licha ya kumuonesha mapenzi.


“Kwako nimepumzika, nimechoka vipigo, dharau, nampenda, unavyotupenda mimi na mwanangu Arina, tunakupenda Sanaa,” alisema Amber Lulu.


Hata hivyo, Amber Lulu hakufichua sura ya mpenzi wake na kuwaacha mashabiki wakitaka kujua ni nani hasa anayetaka jimbo lake?


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii