Mashabiki wa soka Ujerumani wataka kombe la dunia Qatar lisusiwe

Mashabiki wa soka katika viwanja nchini Ujerumani wametoa wito jana Jumamosi, wa kususiwa kwa michuano ijayo ya kombe la dunia nchini Qatar. Mjini Dortmund, mashabiki walionesha bango lisemalo SUSIA QATAR 2022, sambamba na jengine linalosema 'wafu wengi kuliko dakika za kucheza.' Hisia sawa na hizo zilioneshwa na mashabiki wa Bayern Munich na Hertha Berlin katika mchuano wa timu hizo kwenye mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, pamoja na kwenye mchezo wa ligi ya daraja la pili kati ya Fortuna Düsseldorf na St. Pauli. Bango la mashabiki wa Dortmund, lililochapishwa katika rangi za klabu hiyo za njano na nyeusi, lilikuwa linazungumzia dakika 5,760 za kandanda litakalochezwa nchini Qatar, sambamba na idadi vifo vya watu 6,500 inayokuwa ya vibarua walishiriki kazi za maandalizi ya viwanja na miundombinu mengine nchini Qatar kwa ajili ya kombe la dunia. Idadi hiyo iliyochapishwa na gazeti la Uingereza la The Guardian mnamo mwaka 2021 inapingwa vikali na Qatar.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii