SERIKALI ya Afrika Kusini imetaka kusitishwa kwa mnada wa kuuza funguo za chumba cha jela alichokuwa akiishi hayati Nelson Mandela kwenye jela ya “watukutu” ya Robben Island.
Mnada huo uliopangwa kufanyika Jumatatu jijini New York, Marekani utafanya na mlinzi wa zamani wa jela hiyo Christo Brand. Waziri wa utamaduni wa Afrika Kusini, Nathi Mthethwa, amesema serikali ya nchi hiyo haikushirikishwa kwa lolote.
“Ufunguo huu ni wa watu wa Afrika Kusini” amenukuliwa Mthetwa na BBC. “Sio kitu binafsi cha mtu” ameongeza waziri huyo.
Mnada huo unaotarajiwa kufanyika Desemba 28 unalenga kupata fedha kwa ajili ya ujenzi wa bustani ya kumbukumbu na makumbusho kwenye eneo alilozikwa rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.