Cheed na Killy wako huru sasa

Wasanii wa bongo fleva killy na cheed wamethibitisha leo kupitia insta story zao kuwa wako huru kwa sasa kutokana na suala mikataba yao amabayo ili kua na utata na wameeleza kuwapatia mashabiki kile wanachostahili.


Kauli hiyo ya kuwa huru iliyotolewa na Cheed pamoja na Killy ni kufuatia Harmonize jana Jumanne katika ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kuvunja mkataba rasmi kimaandishi na waliokuwa wasanii wake Killy na Cheed.

Ikumbukwe, Cheed na Killy walijiunga rasmi na lebo ya Konde Music Worldwide, Septemba 2020 wakitokea lebo ya King’s Music inayomilikiwa na msanii AliKiba.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii