Mohamed Ali Mohammed Mwenyekiti Mpya UVCCM Taifa

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wamemchagua Mohamed Ali Mohammed (Kawaida) kuwa mwenyekiti mpya wa umoja huo.

Kawaida ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Kusini Unguja anachukua nafasi ya Kheri James ambaye Juni 2021 Rais Samia Suluhu Hassan alimteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo.

Kawaida amepata kura 523 akiwashinda Farid Mohammed Haji aliyepata kura 25, Kassim Haji Kassu kura 2 na Abdallah Ibrahim Natepe aliyepata kura 1.

Akitangaza matokeo hayo Jumapili Novemba 27,2022 Jijini Dodoma msimamizi mkuu wa uchaguzi huo ambaye ni Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alimtangaza Kawaida kuibuka na ushindi huo.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii