NEYMAR AANZA NA MAJANGA

WAKATI timu ya taifa ya Brazil ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Serbia staa wao Neymar alipata maumivu ya enka.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwenye benchi la ufundi la Brazil zimeeleza kuwa hali ya maumivu ambayo amepata itatolewa taarifa kamili baada ya ripoti ya madaktari kutolewa.

Staa huyo baada ya kutolewa alionekana kuwa na masikitiko makubwa akiwa benchi na alikuwa akifarijiwa na wachezaji wenzake kwenye benchi.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Lusail ikiwa ni wa kundi G mabao yote mawili yalijazwa kimiani na Richarlison ilikuwa dakika ya 62 na 73.
Brazil inaongoza kundi hilo kwa sasa ikiwa imekusanya pointi tatu kindindoni.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii