Ndugai achaguliwa kusimamia uchaguzi CCM Dodoma

Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma umemchagu la Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai kuwa mwenyekiti wa muda wa mkutano huo.

Uchaguzi wa Ndugai umekuja kufuatia klanuni ya uchaguzi kwamba mwenyekiti kama anagombea basi atalazimika kupisha nafasi hiyo na mkutano utamchagua mtu mwingine kukalia kiti hicho kuendesha mkutano.


Leo Jumatatu Novemba 21, 2022 mara baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma, Godwin Mkanwa, msimazi alitaka wajumbe wachague mwenyekiti wa muda.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii