Rais aliyetawala kwa muda mrefu zaidi duniani awania muhula mwingine

Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Guinea ya Ikweta anatarajiwa kuendelea kuitawala nchi hiyo baada ya uchaguzi wa Jumapili.

Obiang Nguema ambaye yupo madarakani kwa muda mrefu kuliko kiongozi mwengine yoyote barani Afrika amewania muhula mwingine.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 ametawala kwa muda wa miaka 43 katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta.  Obiang aliingia madarakani mnamo mwaka 1979 baada ya kuuangusha utawala wa rais wa kwanza aliyeingia madarakani tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Uhispania mnamo mwaka 1968.

Katika uchaguzi uliofanyika hapo Jumapili Obiang anatarajiwa kupata zaidi ya asilimia 95 ya kura na hivyo kuendelea na muhula wa sita.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii