WATANZANIA KUPEWA ELIMU YA FEDHA ITAKAYOWASAIDIA KUWA NA UCHUMI IMARA


Kamishna wa uendelezaji wa sekta ya fedha kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Dr Charles Mwamwaja akizungumza na waandishi wa habari juu ya Maadhimisho ya wiki ya Huduma za Fedha yatakayofayika Kitaifa Jijini Mwanza.


Wizara ya Fedha na Mipango imeandaa Maadhimisho ya wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa  kwa wiki moja kwa lengo la kutoa elimu ya fedha kwa Watanzania nchini.


Maadhimisho hayo yatafanyika katika viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza kuanzia Novemba 21 hadi 26 mwaka huu.
Akizungumza leo Novemba 20, 2022 na waandishi wa habari Kamishna wa uendelezaji wa sekta ya Fedha katika Wizara ya Fedha na Mipango Dk Charles Mwamwaja, amesema maandalizi ya Maadhimisho hayo yamekamilika na wakotayari kuwapokea Wananchi kuanzia kesho.


Amesema Maadhimisho hayo yatakuwa ni ya pili kufanyika ambapo ya kwanza yalifanyika Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi mmoja Novemba 8-14 mwaka Jana.


Dk Mwamwaja amesema  elimu ya fedha ni muhimu sana kwani ndio nguzo muhimu ya kuwezesha uchumi wa Watanzania kukua.
Amesema fedha ni rasilimali ya muhimu sana hivyo amewaomba Watanzania kujitokeza kwa wingi ili waweze kupata elimu itakayowasaidia kuwa na matumizi sahihi ya huduma za fedha zinazotolewa ili kujenga uchumi na kuondoa umasikini.


Aidha, ameeleza kuwa mbali na elimu kutolewa wanatarajia kupokea maoni na mawazo mbalimbali kutoka kwa wananchi ili waweze kuboresha huduma zao za kifedha hatua itakayosaidia huduma hizo kuwa rafiki kwa watumiaji.


Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi idara ya hifadhi ya jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Omar Mziya, amesema wamejipanga vizuri katika kuhakikisha elimu ya fedha inawafikia Wananchi.


Nae Meneja wa maendeleo ya soko la Bima kutoka Mamlaka ya usimamizi wa Bima (TIRA) Stella Rutaguza, amesema katika Maadhimisho hayo watatoa elimu ili watu waweze kufahamu umuhimu wa kuwa na Bima.
Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo ” Elimu ya Fedha kwa

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii