Alikuwa na matumaini ya kupona haraka na kurejea kwa timu yake ya Senegal kabla ya kukamilika kwa mechi ya makundi. Kocha Mkuu Aliou Cisse piaa alikuwa amemjumuisha kwenye kikosi chake cha Qatar.
Hata hivyo, Mane alilazimika kujiondoa baada ya kubainika kuwa jeraha lake lingehitaji upasuaji na hivyo kuhitaji muda mrefu zaidi kupona. Jeraha lake bila shaka ni pigo kubwa kwa Senegal ambayo sasa itashiriki michuano ya Kombe la Dunia bila huduma za mchezaji wao nyota.
Mane sasa amewaomba mashabiki kuunga mkono Senegal licha yeye kutoshiriki.
Katika ujumbe uliotumwa kwenye Instagram, mshindi huyo mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika, alitoa taarifa kuhusu upasuaji wake. "Wengi wenu mmetuma ujumbe wa kuniunga mkono kufuatia jeraha langu.
Namshukuru Mungu, upasuaji niliofanyiwa katikati ya wiki ulikwenda vizuri. Nataka kuchukua fursa hii kuwashukuru na kuwaonyesha shukrani zangu kwenu nyote." "Jumatatu hii, nchi yetu pendwa itashiriki Kombe la Dunia, Qatar 2022. Nina hakika Simba itavuka na kukaribia kila mchezo kama fainali ya kweli. Pia nina hakika kwamba Wasenegal wote watakuwa mbele ya skrini ndogo kuunga mkono. na kuhimiza timu yetu ya taifa shujaa. Nina hakika kwamba wachezaji wenzangu watapigana kama mtu mmoja na kama wamezoea kufanya ili kuheshimu Senegal yetu mpendwa."