Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini imewakamata watuhumiwa 9 wakiwa na dawa za kulevya aina ya heroin kg 34.89 ambapo miongoni mwa watuhumiwa hao ni pamoja na Muharami Sultan ambaye ni kocha wa magolikipa wa timu ya Simba na ni mchezaji wa zamani wa timu hiyo pamoja
Muharami Sultan, Kocha wa magolikipa wa timu ya Simba, aliyekutwa na dawa za kulevya na Kambi Zuber Seif maarufu kama Cambiasso.
Mtuhumiwa mwinginie ni Suleiman Matola Said (24) ambaye ni mtoto wa dada yake na mtuhumiwa Kambi Zuberi Seif.
Hayo yameelezwa na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini Kamishna Gerald Kusaya, ambapo watuhumiwa hao wamekamatwa katika oparesheni iliyofanyika kuanzia mwezi Oktoba 2022, hadi mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.