DJ Khaled atinga studio na Burnaboy

Producer maarufu nchini Marekani na duniani kwa ujumla DJ Khaled amekutana na staa wa muziki barani Africa Burnaboy studio na kurekodi baadhi ya nyimbo wakiwa pamoja.


Taarifa za wawili hao kukutana studio zimetoka kwa DJ Khaled mwenyewe baada ya kushea video na picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na Burnaboy studio wakirekodi.

Burnaboy anakuwa msanii mwingine kufanya kazi na wasanii wa Marekani kama alivyofanya Wizkid, Davido na P Square.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii