Arsenal na Manchester United ndio klabu zinazoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi barani Afrika lakini pia katika bara la Asia Manchester wakijatwa kuongoza zaidi.
Mbali na klabu hizo kupitwa kwa wafuasi katika mitandao ya kijamii na klabu kama Real Madrid na Barcelona, kupitia majarida mbalimbali yameeleza kuwa Manchester United na Arsenal zinatajwa kuwa na mashabiki wengi zaidi katika bara la Afrika na Asia zikizipita Real Madrid na Barcelona.
Katika taifa la Nigeria eneo linaloitwa Okene, Kogi State, Nigeria kila mwaka huadhimisha siku ya Arsenal duniani na imeelezwa sherehe hiyo au siku hiyo waliianzisha mwaka 2006.
Mashabiki hao inaelezwa katika sherehe za mwaka huu waliongezeaka mara dufu kutokana na timu yao kufanya vizuri katika michuano mbalimbali barani Ulaya huku wakiongoza ligi, wakiwa juu ya Man City kwa tofauti ya alama moja.