Mkutano huu unafanyika katika wakati hali ya ndani ya China na hali ya kimataifa, ina changamoto mbalimbali kiuchumi na kiusalama, kwa hiyo kitakachojadiliwa na kuamuliwa kwenye mkutano huo, sio kama tu kitakuwa na umuhimu mkubwa kwa China yenyewe, bali pia kitakuwa na umuhimu mkubwa kwa dunia.
Kwa wachina, kinachofuatiliwa zaidi ni kama mafanikio ya kiuchumi, neema na usalama waliokuwa nao katika kipindi cha miaka mitano hadi kumi iliyopita vitalindwa au kuimarishwa na maamuzi yatakayofikiwa kwenye mkutano huo. Kwa watu wengine wa nje ya China, kinachofuatiliwa zaidi ni kama maamuzi ya mkutano huo yatakuwa ya kuijenga China kuwa nchi yenye mchango katika kukabiliana na changamoto za dunia, na kuendelea kuifanya China kuwa moja ya nguzo muhimu za kufufuka kwa uchumi wa dunia na injini ya maendeleo ya dunia.
Kutokana na nafasi ya China katika uchumi wa dunia, mkutano huo umekuwa na ufuatiliaji mkubwa kuhusu mkutano huo karibu katika kila nchi. Hili bila shaka ni shinikizo kwa wajumbe watakaohudhuria mkutano huo, kwa kuwa maamuzi watakayofanya hayatakuwa kwa ajili yao peke yao, chama chao au nchi yao, bali yatagusa dunia nzima. Kwa wanaofuatilia kwa karibu siasa za China na maendeleo yake ya kiuchumi, bila shaka watakuwa wanajua ni nini kimefanyika nchini China katika miaka kumi iliyopita, na mchango binafsi wa Xi Jinping amekuwa na mchango gani katika hayo yaliyofanyika.