Urusi na Belarus kuunda kikosi cha pamoja cha kijeshi

Kiongozi wa Belarus Alexander Lukashenko hapo jana alitangaza kuundwa kwa kikosi cha pamoja cha nchi yake ndani ya jeshi la Urusi. Lukashenko alisema hatua hiyo inatokana na shinikizo linaloongezeka kwenye mpaka kati ya nchi yake na Ukraine, linalolazimu kuimarisha usalama.

Tangazo lake hilo lilikuja wakati Urusi ikivurumusha makombora kuilenga miji mingi ya Ukraine ambayo yaliuwa watu 11 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 60. Lukashenko alisema matayarisho ya kikosi hicho yalianza siku mbili zilizopita wakati mripuko ulipotokea kwenye daraja la Kerch linaloiunganisha Urusi na rasi ya Crimea iliyonyakuliwa kutoka Ukraine mwaka 2014.

Kiongozi huyo ambaye hakutoa maelezo kuhusu watakapopelekwa wanajeshi hao alisema Ukraine ilikuwa ikipanga kuishambulia Belarus. Kauli ya kuundwa kwa kikosi hicho cha pamoja na Urusi imezua wasiwasi kuwa yumkini Belarus inaazimia kuishambulia Ukraine.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii