Burna Boy Aalikwa Paris Kwenye Party ya Beyonce

 BurnaBoy amealikwa kwenye Private Party ya Beyonce, unaambiwa ni watu wachache sana Wamealikwa kwenye party hiyo. Wangekuwa Ndugu zetu wamealikwa tusingepumua.


Hii sio mara ya kwanza Burna Boy Kuwa karibu na Beyonce, kwa wale wajuzi wa mambo nadhani mnaelewa kwamba kuna Album ya Soundtracks zinazopatikana kwenye Filamu ya The Lion King (2019), Album hii ilifanywa na Beyonce na Miongoni mwa Wasanii ambao wameshirikishwa kwenye Album hii ni Burnaboy.


Mbali na Burnaboy, mwanamama Beyoncé aliwapa shavu Wasanii kadhaa kutoka Afrika, Wizkid (Brown skin Girl), Mr Eazi, Yemi, Shatta Wale, Busiswa, Tiwa Savage, Tekno, Etc.


Mashabiki wengi wa Burnaboy baada ya kuona picha hii akiwa na Beyoncé wametamani wawili hawa kufanya Collabo

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii