WATU 90 WAFARIKI BAADA YA ROLI LA MAFUTA KULIPUKA HAITI.


Naibu meya wa mji Cap-Haitien, nchini Haiti Patrick Almonor amesema idadi ya watu waliokufa baada ya lori la mafuta kulipuka wiki iliyopita imeongezeka na kufika watu 90. 


Naibu huyo wa meya anahofia kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka kutokana na majeruhi wengi ambao bado wamelazwa hospitali kufuatia mkasa huo wa moto. 


Kwa mujibu wa ripoti ya awali iliyotolewa na mamlaka ya Haiti, watu 75 walipoteza maisha huku wengine 47 wakiteketea vibaya baada ya lori la mafuta kulipuka wiki iliyopita. Kulingana na Almonor, dereva wa lori la mafuta alipoteza mwelekeo na kusababisha lori hilo kupinduka huku wakaazi wakijaribu kufyonza mafuta yaliyokuwa yamemwagika na baadaye lori hilo kulipuka. 


Nchi hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa mafuta, wakati mwengine mamlaka ikikosa pesa za kuwalipa wauzaji wa mafuta.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii