Museveni Amualika Rais Ruto Uganda Kuadhimisha Siku ya Uhuru

Rais William Ruto anatarajiwa kujumuika katika sherehe za Uhuru nchini Uganda siku ya Jumapili, Oktoba 9, hii ikionekana kama juhudi za kutuliza hali tete iliyoshuhudiwa wiki hii kati ya nchi hizi mbili.


Ripoti zimebainisha kuwa Ruto ni miongoni mwa wageni mashuhuri walioalikwa na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, huku taifa hilo likiadhimisha miaka 60 tangu ijinyakulie uhuru.

Museveni, ambaye amekuwa na uhusiano mwema na Ruto, ametawala Uganda tangu Januari 29, 1986, na kumfanya awe mmoja wa marais Afrika aliyehudumu kwa kipindi kirefu.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii