ZANU-PF yampitisha Mnangagwa kuwa mgombea wake 2023

Chama tawala nchini Zimbabwe ZANU-PF jana Jumamosi kimempitisha Rais Emmerson Mnangagwa kuwa mgombea wake kwa uchaguzi mkuu ujao wa 2023.

Mnangagwa aliingia madarakani 2017 baada ya majenerali wa kijeshi kumlazimisha mtawala wa muda mrefu Robert Mugabe kujizulu. Katika mkutano huo mkuu wa mwaka, ZANU-PF imempa nafasi nyingine Mnangangwa mwenye umri wa miaka 80 muhula mwingine wa miaka mitano kama kiongozi wa chama.

Hata hivyo hakujawa na terehe iliyopangwa kwa uchaguzi wa Zimbabwe ambao umepangwa kufanyika katika nusu ya kwanza ya mwaka 2023.

Mnangagwa alishinda dhidi ya mpinzani wake mkuu Nelson Chamisa katika uchaguzi wa 2018 ulidaiwa kufanyika kwa udanganyifu.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii