KANYE WEST YAMKUTA MAZITO

Makampuni makubwa takribani 5 tayari yamevunja ushirikiano wa kibiashara na Kanye West kufuatia maneno na matamshi yake yenye ukakasi na kudaiwa kujaa chuki na ubaguzi dhidi ya wayahudi, matamshi ya Kanye West yametajwa kuwa sio yenye ubaguzi tu bali yanachochea vitendo vya hatari

Makampuni ambayo tayari yamevunja ushirikiano wa kikazi na Kenye West ni pamoja na Addidas, Balenciaga, GAP, JPmorcan Chase.

Huku, MRC ikisitisha kabisa usambazaji wa documentary mpya kuhusu maisha ya Kanye West iliyokuwa iingie sokoni kufuatia kutibuliwa na maneno yake

CAA ambayo ni agency ya kuwakilisha vipaji iliyokuwa ikifanya kazi na rapa huyo pia imemwaga rasmi

Makampuni karibia yote yanasema suala la ubaguzi au chuki kwenye kundi flani la watu au jamii sio kitu kizuri wala cha kukikalia kimya na wao kama Makampuni wanaamini na kuthamini ushirikiano na ujumuishi

Hii imekuja pia baada ya jarida maarufu na kongwe la Vogue kusitisha ushirikiano wa kikazi na Kanye West kufuatia rapa huyo kumporomoshea maneno mazito mmoja wa wahariri wa jarida hilo aliyekosoa mavazi mapya ya Kanye West katika onesho la mitindo la Paris Fashion Week 2022 ambapo aliwavalisha wanamitindo mavazi yaliyokuwa yakitukuza uzungu na majuzi rapa huyo katika interview kuongea tena maneno yaliyowatibua watu weusi kuhusu kifo cha George Floyd

Hii ni baada ya aliyekuwa mke wa Kanye West yaani Kim Kardashian na familia yake kuonesha wazi walishamchoka rapa huyo kwa drama, vituko na mambo yake ya reja reja Kila leo na kesho ambayo yanatajwa kumharibia taswira yake hata yeye mwenyewe

Aidha, baadhi ya marafiki wa Kanye West wamesema rapa huyo anaonekana wazi hayupo sawa kwasasa anatakiwa kupewa msaada


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii